/*Start Css Menu*/ .menu{ border:none; border:0px; margin:0px; padding:0px; font-family:verdana,geneva,arial,helvetica,sans-serif; font-size:14px; font-weight:bold; color:8e8e8e; } .menu ul{ background:url(https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj03EcWc5W014Naf0PEVAwQmPj0NilOTBFokErgDzpKBSM3PcUhdpFPufauMGuSrIP0Q5WDrsQr87KWjEm3uhgqnlpekyYkqfczcVa73Uw39gXT2Xywo28v_kCQ4qEBuoykiVYUiM3sQKE5/s1600/menu-bg.gif) top left repeat-x; height:43px; list-style:none; margin:0; padding:0; } .menu li{ float:left; padding:0px 8px 0px 8px; } .menu li a{ color:#666666; display:block; font-weight:bold; line-height:43px; padding:0px 25px; text-align:center; text-decoration:none; } .menu li a:hover{ color:#000000; text-decoration:none; } .menu li ul{ background:#e0e0e0; border-left:2px solid #a80329; border-right:2px solid #a80329; border-bottom:2px solid #a80329; display:none; height:auto; filter:alpha(opacity=95); opacity:0.95; position:absolute; width:225px; z-index:200; /*top:1em; /*left:0;*/ } .menu li:hover ul{ display:block; } .menu li li { display:block; float:none; padding:0px; width:225px; } .menu li ul a{ display:block; font-size:12px; font-style:normal; padding:0px 10px 0px 15px; text-align:left; } .menu li ul a:hover{ background:#949494; color:#000000; opacity:1.0; filter:alpha(opacity=100); } .menu p{ clear:left; } .menu #current{ background:url(https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh1zPsUwcLYjxDiCcFFwwzmyMEWKilgj7SwJxPHKzjo1RG4Mdo_jsiZrpLKarpC8AQ2YC9eX0YfPlhJ-JJKRwo7HkLr1rV-8f5bTFTe2-LSi0a63063jIwNa2judRIAk_cFPwdZbHAITN8g/s1600/current-bg.gif) top left repeat-x; color:#ffffff; } /*End Css Menu from http://www.spiceupyourblog.com*/

Powered by Blogger.

Tuesday, July 31, 2012

MSANII NASEEB ABDUL A.K.A DIAMOND PLATNUM YUPO HOI KITANDANI!!

Hii ni picha ya Diamond akiwa hospitali baada ya kubanwa ghafla na kifua na
hivyo kwenda kufanyiwa uchunguzi ili kujua tatizo. Kwa mujibu wa Ommy
Dimpoz ambaye ni mshikaji wake wa karibu tayari msanii huyo
amesharuhusiwa lakini majibu ya vipimo vyake yatatoka kesho.
Miezi ya hivi karibuni Diamond amefululiza kufanya show katika mikoa
mbalimbali bila kupata mapumziko ya kutosha na huenda hiyo ndio ikawa ni
sababu. Kupitia Twitter Diamond ameandika "Dah hali yangu si nzuri, naumwaaa."
Tunamwombea Diamond apone haraka.


BAADA YA YANGA KUZUBAA SASA,MRISHO NGASSA KUTUA SIMBA !!

  BONGO SWAHILI.....Imelipata tamko rasmi la azam kuhusiana na sakata la mchezaji wao anayeonesha mapenzi ya wazi na yanga ambayo ndio mabingwa wa kagame cup
Club ya azam yatoa tamko kuhusu ngasa kupitia ukurasa wao wa facebook "Azam FC
Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa rasmi kuwa baada ya baada ya mchezaji wetu Mrisho Ngasa kuonesha wazi kuwa na mapenzi na Yanga kwa kuivaa na kuipiga busu Logo ya Yanga, tuliwapa Yanga nafasi ya upedeleo ya kumnunua lakini hadi leo hakuna ofa iliyokuja toka Yanga. simba wametoa ofa na uongozi unatafakari ofa ya Simba
Yanga.... Ngasa anauzwa $50,000 wadau wa Yanga tunajua mnampenda sana Ngasa... fikisheni ujumbe kwa uongozi wenu...." 

Saturday, July 28, 2012

Friday, July 27, 2012

MWANAMUZIKI CHAMELEONE AONEKANA MZUSHI!!

      DJ mkongwe nchini, John Dilinga Matlou ‘DJ JD’, leo nae ameweka wazi utapeli aliowahi kufanyiwa miaka saba iliyopita na mwanamuziki raia wa Uganda, mwenye hulka ya utapeli, Joseph Mayanja Chameleone.
JD, amewaeleza waandishi wa habari leo, waliokusanyika kwenye Hoteli ya The Atriums kwamba Chameleone siyo mtu mzuri anapokubaliana na mapromota, kwani hata yeye aliwahi kumtapeli dola za kimarekani 3,000, mwaka 2005.
Alisema mbele ya waandishi wa habari: “Niliwasiliana na Chameleone moja kwa moja, akanikubalia kwenye tamasha langu lililokuwa linaitwa Wakilisha. Nilimlipa dola 3,000, baada ya kupokea fedha, hakuonekana tena na hata simu yangu akawa hapokei.
“Aliendelea kunikimbia hivyo. Tatizo kubwa lipo kwa mapromota wa Kitanzania, hatuna ushirikiano kabisa. Kila alipokuja nchini kufanya shoo, nilimfuata promota husika lakini promota mwenyewe alimficha Chameleone asikamatwe.
“Mwaka 2006, Chameleone alikuja nchini kwenye shoo fulani. Kama kawaida yake alijitahidi sana kujificha nisimfikie. Hata hivyo, pamoja na kujificha kwake, nilipewa taarifa usiku kwamba yupo Bilicanas. Nikawataarifu polisi tukaenda kumkamata.
“Chameleone aliponiaona alinikimbia. Ndugu zangu, Chameleone alikimbia kama mwizi. Pale Bilicanas walikuwepo Rita Paulsen wa BSS na Merey Balhabou. Wakati polisi wamemkamata, Chameleone alikubali namdai dola 3,000 na akakubali kulipa.
“Kusikia hivyo, Rita na Merey wakaniomba nimsamehe kwa sababu mtu mwenyewe amekubali kulipa. Nikawaambia ameshanisumbua sana, Merey akasema kama hatalipa, basi yeye atamlipia. Akanisihi sana kuwa mimi ni mtu wa Morogoro mwenzake, kwa hiyo nimuache Chameleone.
“Nilikubali walichokisema lakini kuanzia hapo, Chameleone na Merey hawakupatikana. Merey alikuwa ‘bize’ na mambo yake, wakati Chameleone hakutaka kupokea simu yangu kabisa.
“Siku moja nilibadilisha namba ya simu nikampigia Chameleone, akapokea vizuri. Nikamkumbusha kuhusu fedha zangu, akaniambia hana uwezo wa kulipa ila anachoweza kufanya ni mimi kuandaa shoo nyingine halafu yeye atakuja ku-perform.
“Pamoja na kuahidi, kila nilipoandaa shoo, ukifika muda wake wa kuja hakufanya hivyo. Hii inamaanisha kuwa Chameleone ana tabia ya utapeli na Watanzania tunapaswa kuwa wamoja kwenye hili tatizo.”
JD alisema, ameamua kutokeza na kueleza haya kipindi hiki ili kila mtu atambue kwamba Chameleone siyo mtu mzuri kwenye fedha na anaweza kumkana promota wakati wowote.