DJ
mkongwe nchini, John Dilinga Matlou ‘DJ JD’, leo nae ameweka wazi
utapeli aliowahi kufanyiwa miaka saba iliyopita na mwanamuziki raia wa
Uganda, mwenye hulka ya utapeli, Joseph Mayanja Chameleone.
JD, amewaeleza waandishi wa habari leo, waliokusanyika kwenye Hoteli ya
The Atriums kwamba Chameleone siyo mtu mzuri anapokubaliana na
mapromota, kwani hata yeye aliwahi kumtapeli dola za kimarekani 3,000,
mwaka 2005.
Alisema
mbele ya waandishi wa habari: “Niliwasiliana na Chameleone moja kwa
moja, akanikubalia kwenye tamasha langu lililokuwa linaitwa Wakilisha.
Nilimlipa dola 3,000, baada ya kupokea fedha, hakuonekana tena na hata
simu yangu akawa hapokei.
“Aliendelea
kunikimbia hivyo. Tatizo kubwa lipo kwa mapromota wa Kitanzania, hatuna
ushirikiano kabisa. Kila alipokuja nchini kufanya shoo, nilimfuata
promota husika lakini promota mwenyewe alimficha Chameleone asikamatwe.
“Mwaka 2006, Chameleone alikuja nchini kwenye shoo fulani. Kama kawaida
yake alijitahidi sana kujificha nisimfikie. Hata hivyo, pamoja na
kujificha kwake, nilipewa taarifa usiku kwamba yupo Bilicanas.
Nikawataarifu polisi tukaenda kumkamata.
“Chameleone
aliponiaona alinikimbia. Ndugu zangu, Chameleone alikimbia kama mwizi.
Pale Bilicanas walikuwepo Rita Paulsen wa BSS na Merey Balhabou. Wakati
polisi wamemkamata, Chameleone alikubali namdai dola 3,000 na akakubali
kulipa.
“Kusikia
hivyo, Rita na Merey wakaniomba nimsamehe kwa sababu mtu mwenyewe
amekubali kulipa. Nikawaambia ameshanisumbua sana, Merey akasema kama
hatalipa, basi yeye atamlipia. Akanisihi sana kuwa mimi ni mtu wa
Morogoro mwenzake, kwa hiyo nimuache Chameleone.
“Nilikubali
walichokisema lakini kuanzia hapo, Chameleone na Merey hawakupatikana.
Merey alikuwa ‘bize’ na mambo yake, wakati Chameleone hakutaka kupokea
simu yangu kabisa.
“Siku
moja nilibadilisha namba ya simu nikampigia Chameleone, akapokea
vizuri. Nikamkumbusha kuhusu fedha zangu, akaniambia hana uwezo wa
kulipa ila anachoweza kufanya ni mimi kuandaa shoo nyingine halafu yeye
atakuja ku-perform.
“Pamoja
na kuahidi, kila nilipoandaa shoo, ukifika muda wake wa kuja hakufanya
hivyo. Hii inamaanisha kuwa Chameleone ana tabia ya utapeli na
Watanzania tunapaswa kuwa wamoja kwenye hili tatizo.”
JD
alisema, ameamua kutokeza na kueleza haya kipindi hiki ili kila mtu
atambue kwamba Chameleone siyo mtu mzuri kwenye fedha na anaweza kumkana
promota wakati wowote.
0 comments:
Post a Comment