Nikafanikiwa kusoma chuo na kwenda nchini Afrika Kusini kusomea sheria, nilifurahi sana. Sikutaka kurudi nyumbani, nikaoa huko huko na kupata watoto. Katika maisha yangu yote hayo hakika sikumkumbuka kabisa mama yangu, nilikuwa nikitamani
sana afe ili niwe na furaha. Nikafanikiwa kupata watoto wawili huku nikiwa nimejenga nyumba ya kifaari na kuwa na utajiri mkubwa. Kuna
siku nikasikia mlango ukigongwa, watoto wangu wakaenda kuufungua mlango,
ALIKUWA NI MAMA YANGU amekuja kunitembelea. Watoto wangu wakaanza kulia kwani walikuwa wakimuogopa sana mama yangu kutokana na hali ya kukosa jicho aliyokuwa nayo, nikaamua kwenda mlangoni, nilipomuona, alifikiri ningetabasamu, nikamfokea kwa haira sana "TOKA NYUMBANI
KWANGU KINYAGO CHA MPAPURE WEWE UNAWATISHA WATOTO WANGU". Kwa sauti iliyojaaupole, mama yangu akaniambia "SAMAHANI BABA. NAFIKIRI
NITAKUWA NIMEKOSEA NJIA" hapo hapo akaondoka. Nikafanikiwa kutembelea nchini
Tanzania, na moja kwa moja nikaanza kwenda kwenye nyumba ile tuliyokuwa tunakaa. Majirani zangu wakaniambia kuwa mama yangu alikuwa amefariki kwa kuwa tundu la jicho lake lilikuwa limeharibu hadi mishipa ya fahamu, WALA SIKUHUZUNIKA KABISA ZAIDI YA KUTABASAMU. Hapo ndipo waliponiletea barua ambayo aliiandika mama yangu na kunipa. Barua ile ilikuwa imeandikwa hivi.
' Mwanangu mpendwa.
Najua kwamba katika maisha
yako ulikuwa ukinichukia sana ila amini kwamba nilikuwa
nikikupenda sana. Ulipokuwa
mtoto ulipata ajali, jicho lako
likapasuka ila kwa kuwa nilikuwa
sitaki uishi maisha ya kuwa na
jicho moja, nikaamua kutoa jicho langu na kuwekewa wewe ili tu
uweze kuuona ulimwengu kwa
macho yote mawili. Sikutaka
kujali ningepata matatizo gani
lakini niliamini kwamba wewe
ndiye ungekuwa furaha yangu hasa kila nitakapokuona
unauangalia ulimwengu huu
huku ukitumia jicho langu moja.
Mimi mama yako Mpendwa.
Daaaaaaahhhh!!! mama ni mama jamani hata kama ni chonge atabaki kuwa mama yako tu!!!! usimdhalau mzazi kamwe hata ukipata mafanikio ya aina gani ila kama utamdharau mama hakika mafanikio yako si kitu katika Dunia
ReplyDeletemajuto n mjukuu pole kijana
ReplyDelete