Wednesday, August 1, 2012
OFFICIAL:MRISHO NGASSA SASA ATUA RASMI SIMBA!!
Hatimaye klabu ya Azam FC ya Tanzania imemuuza mshambuliaji wake Mrisho Khalfan Ngassa kwenda klabu ya Simba SC.
Azam
ambao walimsaini Ngassa kwa ada iliyovunja rekodi ya uhamisho kwa
wachezaji wanaocheza Bongo, Million 55, wamemuuza Ngassa kwa ada ya
millioni 25 iliyolipwa cash na mabingwa wa Tanzania Simba.
Akizungumza
na mtandao huu meneja wa Azam, Patrick Kahemele amesema kamati ya
ufundi ya klabu pamoja na uongozi walikubalina kumuweka sokoni Mrisho
Ngassa mara tu baada ya kumalizika kwa michuano ya Kagame Cup ambayo
iliisha kwa Azam kushika nafasi ya pili nyuma ya Yanga.
"Klabu
iliamua kumweka sokoni Ngassa mara tu baada ya michuano ya Kagame
kumalizika, kwa kuwa mwenyewe alionesha nia ya kujiunga na klabu yake ya
zamani Yanga, sisi tuliwapa kipaumbele Yanga, lakini pia Simba nayo
ilionesha nia ya kumtaka. Tukafungua bid na kutangaza tunahitaji
$50,000. Yanga baada ya kuwajulisha juu ya hili wakatuma ofa ya millioni
20, Simba nao wakatuma millioni 25. Ofa zote zilikuwa chini ya kiasi
tulichohitaji lakini baada ya majadiliano ya viongozi wote wa Azam
tukaona bora tumuuze tu, kwa bei ya millioni 25.
"Kwa kuwa
Simba walikuwa wameshafikia viwango na sisi lengo letu lilikuwa ni
kumuuza Yanga, asubuhi ya leo tukawatumia email Yanga tukiwaambia
waboreshe ofa yao na tukawaambia bid ya Ngassa itafungwa saa saba
mchana, lakini hadi muda huo unafika Yanga hawakuwa wametujibu chochote,
kitendo ambacho tulikitafsiri hawana nia ya dhati ya kumsaini mchezaji
huyo, kwa upande mwingine Simba walikuwa tayari wamefikia dau
tulilolitaka hivyo tukafunga bid na kumuuza mchezaji huyo kwa Simba,"
alimaliza Patrick.
Tunaendelea kumtafuta Mrisho Ngassa na pale tutakapompata tutawaletea taarifa rasmi kuhusu alivyopokea taarifa za kuuzwa Simba.
By Aidan Charlie
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment