Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Vodacom kwa kuja
na wazo zuri la kutambua michango na umuhimu wa mitandao ya kijamii,
hususan blogs na web site na kuamua kuwatunuku.
Pamoja na pongezi
hizo, lakini mmekosea katika utekelezaji wake. Kwa mtizamo wa wahusika
wengi (Blogers), tuzo mlizotoa baadhi zimeenda kwa wasiostahili na
mmeacha wengi waliostahili kupata tuzo hizo.
Ingawa hamkuweka wazi
vigezo vyote, lakini baadhi ya mlivyovitaja ni pamoja na blog kuwa
inayofanyakazi (active), ambayo inaweka habari mpya kila siku, iwe
inayoandika vitu halisi na siyo vya kukopi au kutafsiri kutoka BBC na
mitandao mingine ya Kiingereza na kupesti.
Hali kadhalika mkasema
kuwa web site au blog hiyo inachokiandika kiwe kimeandikwa na mtu mwenye
ujuzi nacho, mkatoa na mfano kuwa kama ni mapishi, basi yaandikwe na
mtu mwenye kujua mapishi. Pia mtandao huo uwe maarufu.
Bila shaka
kwenye ulimwengu wa mitandao, unaposema mtandao fulani ni maarufu, ina
maana unatembelewa na visitors wengi kwa siku, mtandao hauwezi kuwa
maarufu kisha ukawa na visitors 500 au 800 tu kwa siku.
Bloggers
maarufu nchini wanajuana na wanahesabika, inakuwa kichekesho inapokuja
kutangazwa blog fulani ndiyo maarufu wakati haijulikani hata miongoini
mwa bloggers wenyewe, achilia mbali wasomaji wengine.
Hawa ndiyo washindi wenyewe:
- Mikocheni Report,
- Issa Michuzi
- Wanamuziki Tanzania.
- Kipanya.co.tz
- Vijana FM
- Millardayo.com
- Taste of Tanzania
- Jamii Forums
- Mambo Magazine
- DJ Fetty Blog
Kwa mtizamo wa wengi, katika orodha hiyo ya
watu kumi, ni wanne tu ndiyo walistahili na waliobaki hawakustahili
kabisa, kwa sababu licha ya kuwa hawajulikani sana, lakini pia huoni
hata namna ambavyo Vodacom, kama kampuni, inaweza kunufaika nao iwapo
mtaamua kujitangaza kupitia kwao.
Kuna Bloggers wameachwa ambao wao
ku blog ndiyo maisha yao, wanalala, wanaamka, wanatembea, wanakula,
wanakunywa, wanakaa wana blog tu. Wao na Blog, Blog na wao. Hakuna
taarifa, breaking news au picha za matukio yote muhimu zinazowapita hapa
nchini na hata katika kuripoti matukio ya promosheni ya Vodacom kwenye
mitandao yao wako mstari wa mbele. Wengine kazi yao ni kukopi na kupesti
kazi za wengine!
Pengine hatuyajui malengo ya Vodacom, kwa sababu
kama kweli mnanataka kuthamini michango ya 'social media' na wao
kunufaika na media hizo, basi mmekosea katika hili.
Waulizeni
mliowatuma, wamefanya research ya kutosha na kuona hao washindi wana
visitors wangapi na pageviews ngapi kwa siku? Je, Google Analytics
Report zao zinaoneshaje? Na, je, habari na picha wanazoziweka kwenye
mitandao yao, kweli ni za kwao, au wamekopi na kupesti tu kutoka
kwingine?
Naomba mliopewa kazi ya kuandaa tuzo hizi myachukue haya
kama changamoto na kuyafanyia kazi ili msiharibu kazi nzuri inayofanywa
na Vodacom nchini Tanzania na wala hatuyasemi haya kwa sababu ya chuki
binafsi, bali kwa ukweli na uwazi tu!
Wassalaam!
Global Publisherstz.com