Klabu ya Azam FC inapenda kutoa taarifa kuwa mkataba wake na kocha
Stewart John Hall kutoka nchini uingereza ulisitishwa rasmi jana Tarehe
31/07/2012 kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Klabu ya Azam FC inajivunia mafanikio ya kocha Stewart Hall, na
inampongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya katika muda wote aliofanya kazi
kama kocha mkuu na mkurugenzi wa ufundi.
Chini ya Stewart Hall, Azam FC ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mapinduzi
Cup, Kushika nafasi ya pili katika ligi kuu, Mashindano ya Urafiki na
Kombe la kagame. Haya ni mafaniko ambayo hayajawahi kufikiwa na makocha
wote waliotangulia na ni mafaniko ya kihistoria katika klabu ya Azam FC.
Azam FC inamtakia kocha Stewart Hall kila la heri, na inatarajia kuwa
ipo siku katika siku za usoni kocha Stewart atarudi tena kufanya kazi na
Azam FC.
Stewart Hall anaacha changamoto kubwa sana kwa mrithi wake ambaye
atatangazwa hapo baadaye lakini kizuri ni kuwa, mrithi wa Stewart Hall
atakuwa ni mwalimu anayefuata mfumo ule ule wa uchezaji ulioachwa na
Stewart Hall kwani hiyo ndiyo (Playing Philosophy ya Azam FC)
Kwa sasa timu itakuwa chini ya Vivek Nagul na Kally Ongala
Imetolewa na Utawala
Azam FC
Ndugu Waandishi, Nalazimika kukutana nanyi kutoa maelezo juu ya tuhuma zenye shinikizo la kisiasa zinazoelekezwa kwangu binafsi kwamba ...
Followers
Blogger news
About Me
Natambua kuwa una kazi nyingi za kukupatia kipato na kujenga taifa. Hata hivyo majukumu yako hayakuzuii kupata habari na burudani! Hii ndiyo sababu nikaanzisha Blog hii ambayo itakufuata popote ulipo. Hapa utapata Makala za Burudani, Simulizi za Mapenzi,Makala za Uhusiano, Meseji kali za Mapenzi, Chemsha Bongo pamoja na Habari za Burudani za Mastaa wa hapa Bongo. Kubwa zaidi ni kukupa mengi yahusuyo Uhusiano,Mapenzi pamoja na udaku. Maoni yako ni muhimu sana. Tafadhali nitumie comments zako baada ya kusoma kazi husika. Lengo ni kuboresha zaidi. KARIBUNI MARAFIKI!!
Habari kubwa Magazetini Kenya leo January 22, 2024
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania January 22,
2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na
za nyuma Magazetini...
0 comments:
Post a Comment